15.1 C
New York

Skendo kubwa zilizotikisa ulimwengu wa michezo

Published:

LONDON, Uingereza

KLABU ya Manchester City iko kikaangoni kwa tuhuma za kukiuka sheria ya Nidhamu ya Matumizi ya Fedha lakini hii si skendo ya kwanza katika ulimwengu wa soka.

Bingwa zamani wa mchezo wa mbio za baiskeli, Lance Armstrong, aliwahi kutikisa dunia kwa skendo yake ya kutumia dawa za kuongeza nguvu akiwa na mataji saba ya michuano ya Tour de France.

Aidha, staa wa kriketi wa Afrika Kusini, Hansie Cronje, naye aliwahi kuingia kwenye skendo kubwa ya kupanga matokeo.

Cronje angeweza kuwaita wachezaji wenzake wa timu ya taifa ya kriketi ya Afrika Kusini kuwaambia kuwa kuna ofa ya pesa nyingi endapo wangekubali kupoteza mchezo.

Moja ya mechi alizowahi ‘kuuza’ ni ile iliyozikutanisha Afrika Kusini na England mwaka 2000, ambapo Cronje aliripotiwa kuvuna kitita cha Pauni 5,000.

Mwanzoni mwa mwaka 2000, baada ya Cronje kukiri kujihusisha na upangaji wa matokeo, alifungiwa Maisha kujihusisha na kriketi. Alifariki miaka miwili tu baadaye kwa ajali ya ndege akiwa na umri wa miaka 32.

Skendo nyingine kubwa kuwahi kutokea katika ulimwengu wa michezo ni ile ya Juventus kushuka Daraja, kutoka Ligi Kuu [Serie A] hadi Daraja la Pili [Serie B]. Hiyo ilikuwa mwaka 2004.

Ni skendo iliyozihusisha pia klabu za AC Milan, Fiorentina na Lazio na klabu zote zilikatwa pointi, huku Juventus ikishushwa Daraja.

Kushuka daraja kuliifanya Juventus ipoteze baadhi ya mastaa wake, wakiwamo Zlatan Ibrahimovic na Patrick Vieira waliotimkia Inter Milan, Fabio Cannavaro na Emerson waliokimbilia Real Madrid, Lilian Thuram na Gianluca Zambrotta waliosajiliwa na Barcelona, na Adrian Mutu aliyejiunga na Fiorentina.

Baadhi ya mastaa waliokubali kushuka na timu ni pamoja na Gianluigi Buffon, Alessandro del Piero, Giorgio Chiellini, Pavel Nedved na David Trezeguet.

Related articles

Recent articles