18.8 C
New York

Yanga nyumbani, Simba wao ugenini

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini

KILA mtu ashinde zake! Katika mechi nne walizocheza wakiwa nyumbani msimu huu wa Ligi Kuu Bara, mabingwa watetezi, Yanga, wameshinda zote, hivyo kukusanya pointi zote 12.

Kwa upande wa wapinzani wao wakubwa katika mbio za ubingwa, Simba, wao nao wamekuwa moto kwenye viwanja vya ugenini, ambapo wameshinda mechi zote nne.

Yanga, katika mechi za ugenini, wameshinda zote mbili, kama ambavyo Simba imefanya kwenye michezo yao ya nyumbani.

Ikimaanisha, si Yanga wala Simba iliyoonja kichapo katika mechi zake sita za msimu huu wa Ligi Kuu Bara, ambayo kwa sasa imesimama kupisha kalenda ya FIFA [Shirikisho la Soka la Kimataifa].

Aidha, Simba ‘Wekundu wa Msimbazi’ wakiwa ugenini wamefunga jumla ya mabao nane na kuruhusu moja, wakati Yanga ‘Timu ya Wananchi’ wamepachika matano na kufungwa moja.

Wakati huo huo, kwa upande wa michezo ya nyumbani, Yanga imefunga mabao 11 na kufungwa moja, huku Simba ikiwa na mabao matatu ya kufunga ikiwa haijaruhusu nyavu zake kutikiswa.

Related articles

Recent articles