Na Hassan Mwasha, Gazetini
SIKIA hii! Usichokijua ni kwamba TRA United ya mkoani Tabora ndiyo timu inayoongoza kwa idadi kubwa ya sare kufikia hatua hii ya msimu huu wa 2026-27 wa Ligi Kuu Bara.
TRA United wameingia kwenye mapumziko ya kupisha kalenda ya FIFA wakiwa na sare tatu katika mechi zao sita walizoshuka dimbani kwenye Ligi, wakishika nafasi ya 12 kwenye msimamo.
Kwa mwenendo walionao katika mechi tatu zilizobaki, wakali hao wameshinda moja [3-1 dhidi ya Pamba Jiji] na kuchezea vichapo viwili, hivyo kukusanya jumla ya pointi sita pekee.
Wakati huo huo, matajiri wa Chamazi, Azam FC, na wakali wa Bukoba, Kagera Sugar, zinafuata kwa kuwa na sare nyingi, ambapo kila moja imepata mbili.
Hata hivyo, licha ya sare hizo, Azam iko nafasi ya pili kwenye msimamo kwani imeshinda mechi nne na kufungwa moja, ingawa imeshashuka dimbani mara saba. Kagera yenye mechi sita, haijashinda, bali imefungwa nne na iko nafasi ya 15.
Je, timu hizo zitarudi na sura tofauti baada ya kumalizika kwa mapumziko ya kupisha mechi zilizopo kwenye kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa [FIFA]?


