LAGOS, Nigeria
CHANZO cha kifo cha rafiki wa karibu wa staa Davido, Ego, kimetajwa kuwa ni operesheni ya kuongeza ukubwa wa umeme wake aliyofanyiwa Machi, 2026, huko Thailand.
Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, Ego alipoteza maisha akiwa kwenye hoteli moia mjini Bangkok baada ya kufanyiwa operesheni hiyo.
Akiwa hapo, mshikaji huyo mwenye umri wa miaka 43 alimwambia mkewe kuwa anahisi maumivu makali ya kifua, ndipo alipokimbizwa katika Hospitali ya Sukhumvit.
Baada ya kuwekwa chumba maalumu cha wagonjwa mahututi, madaktari walibaini kuwa alipata tatizo la mishipa ya damu kuziba kwenye mapafu.
Vipimo vya baada ya kifo chake vilibaini kuwa chanzo cha tatizo ni asidi iliyotumika katika operesheni yake nchini Thailand. Alizikwa London, Uingereza.


