NIAMEY, Niger
WANANCHI wa Niger wamelala usiku wa kuamkia leo wakiwa na hofu baada ya milio ya risasi na risasi na bunduki kusikika mjini Niamey.
Washambuliaji waliotajwa kuwa ni waasi walilenga Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Diori Hamani, ambao pia una kambi ya jeshi ndani yake.
Kwa mujibu wa taarifa zilizoripotiwa na vyombo mbalimbali vya habari, waasi hao walijaribu pia kufyatua mitego ya ulinzi katika makazi ya Rais.
Niamey, Mji Mkuu wa Niger, umelengwa mara mbili na mashambulizi ya kigaidi tangu mwaka huu uanze.
Makundi yanayoyumbisha hali ya usalama nchini humo ni Dola ya Kiislam ya Sahel (EIS) na Kundi la Kusaidia Uislam na Waislam (JNIM).
Niger, kama ilivyo kwa majirani zao, Mali na Burkina Faso, iko chini ya utawala wa kijeshi lakini hali ya usalama imeendelea kuwa mbaya katika maeneo mengi ya nchi hiyo.


