Miami, Marekani
KAMPUNI ya utengenezaji na usambazaji wa vifaa vya michezo ya Adidas ndiyo iliyoongoza kwa kuhudumia timu nyingi wakati wa fainali za Kombe la Dunia zilizomalizika jana Julai 19, 2026.
Kwa mujibu wa mtandao wa Tonton Sports, Adidas ilisambaza jezi zake kwa timu 14, ikifuatiwa na kampuni zingine mbili zilizofanya vizuri – Nike (12) na Puma (11).
Kwa ujumla, kampuni tatu hizo zilihudumia timu 37 kati ya 48 zilizoshiriki fainali za mwaka huu (2026) zilizofanyika Marekani, Mexico na Canada.
Timu zilizochagua kuhudumiwa na Adidas ni Algeria, Argentina, Ubelgiji, Colombia, Curaçao, Ujerumani, Japan, Mexico, Qatar, Saudi Arabia, Scotland, Afrika Kusini, Hispania, na Sweden.
Kwa upande wa Nike, ni Australia, Brazil, Canada, Croatia, England, Ufaransa, Uholanzi, Norway, Korea Kusini, Uturuki, Marekani, na Uruguay.
Puma ilifanya kazi na Austria, Czech, Misri, Ghana, Ivory Coast, Morocco, New Zealand, Paraguay, Ureno, Senegal, na Uswis.
Aidha, ipo kampuni ya Kelme, ambayo ilizihudumia timu mbili – Bosnia na Jordan, katika fainali hizo.
Kampuni zingine zilizohudumia timu moja moja ni Capelli (Cape Verde), Umbro (DRC), Marathon (Ecuador), Saeta (Haiti), Majid (Iran), Jako (Iraq), Reebok (Panama), Kappa (Tunisia), na 7Saber (Uzbekistan).


