21.4 C
New York

Ufaransa yaweka rekodi mbaya Kombe la Dunia

Published:

MIAMI, Marekani 

KATIKA kipigo cha mabao 6-4 kutoka kwa England, timu ya soka ya Taifa ya Ufaransa imeweka rekodi mbaya zaidi kuwahi kuwakuta katika miaka 58 iliyopita.

Kwa mara ya kwanza tangu miaka 58 iliyopita, Ufaransa ilikubali kuruhusu mabao manne ndani ya kipindi cha kwanza katika mechi ya ushindani.

Ukiwa ni mchezo wa kusaka mshindi wa tatu, Ufaransa iliruhusu mabao manne hayo katika dakika ya 3 (Declan Rice), 18 (Ezri Konsa), 37 na 45 (Bukayo Saka).

Mara ya mwisho kwa ‘Les Bleus’ kufungwa mabao manne kabla ya mapumziko ilikuwa mwaka 1968 walipokutana na Yugoslavia.

Kwa mujibu wa historia, hiyo ilikuwa mechi ya kuwania tiketi ya kushiriki fainali za Mataifa ya Ulaya (EURO).

Related articles

Recent articles