21.4 C
New York

Mastaa hawa Kombe la Dunia limewapa kiki Instagram

Published:

MIAMI, Marekani

KWA kipindi cha mwezi mmoja wa michuano ya Kombe la Dunia msimu huu wa 2026, Erling Haaland ameongeza wafuasi milioni 29 katika akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa Instagram.

Kwamba kwa sasa ana wafuasi zaidi ya milioni 70, akitarajiwa kufikisha milioni 322 kufikia mwishoni mwa mwaka 2026.

Wakati huo huo, kipa wa timu ya soka ya Taifa ya Cape Verde, Vozinha, amezoa wafuasi wapya takribani milioni 5 kwa kipindi hiki tu cha Kombe la Dunia.

Kwa sasa, kaunti ya Instagram ya kipa huyo mwenye umri wa miaka 40 ina wafuasi 29.3.

Jude Bellingham wa England naye amenufaika vilivyo na Kombe la Dunia, akiongeza wafuasi takribani milioni 9 ndani ya mwezi mmoja wa michuano hiyo.

Ni kama ilivyo kwa staa wa Hispania, Lamine Yamal, ambaye ameongeza idadi kubwa ya wafuasi na kufikia milioni 49.6 huko Instagram.

Naye beki wa New Zealand, Tim Payne, alikuwa na wafuasi wasiozidi 500,000 kabla ya kuanza kwa fainali za Kombe la Dunia za mwaka huu.

Hata hivyo, katika kipindi cha mwezi mmoja wa mashindano, ameweza kufikisha wafuasi milioni 5.8 kwenye akaunti yake ya Instagram.

Related articles

Recent articles