LONDON, Uingereza
KLABU ya Real Madrid imefikia makubaliano na beki wa Chelsea, Marc Cucurella, na huenda akatua Santiago Bernabeu baada ya Kombe la Dunia.
Cucurella (27), yuko kwenye michuano hiyo huko Marekani, Mexico na Canada akiwa na timu ya Taifa ya Hispania.
Kwa mujibu wa ripoti, Madrid chini ya Rais aliyerudi madarakani, Florentino Perez, imetenga Pauni milioni 43 kumnasa nyota huyo.
Ikumbukwe, Madrid imeshatangaza kumrejesha kocha Jose Mourinho kwa mkataba wa miaka mitatu.
Wakati huo huo, bado inahusishwa na kiungo wa Manchester City, Bernardo Silva, beki wa Inter Milan, Denzel Dumfries, na staa aliyeondoka Liverpool, Ibrahima Konate.


