19.8 C
New York

Carrick, Man United na safari ya matumaini 2025-26

Published:

MANCHESTER, Uingereza

RUBEN Amorim alitimuliwa kwenye benchi Januari, 2026, na nafasi yake kuchukuliwa na kocha Michael Carrick, ambaye ameiwezesha Manchester United kurejea Ligi ya Mabingwa.

Ni baada ya Man United kumaliza msimu wa Ligi Kuu ya England (EPL) ikiwa nafasi ya tatu kwenye msimamo, nyuma ya mabingwa Arsenal na Manchester City.

Hata hivyo, Man United imemaliza msimu ikiwa haina taji lolote. Iliishia raundi ya tatu Kombe la FA na raundi ya pili EFL Cup.

Kwa ujumla, ‘Mashetani Wekundu’ walifunga mabao 72 katika michuano yote, pia wakiruhusu nyavu zao kutikiswa mara 54.

Katika mechi 17 alizokaa kwenye benchi, Carrick alishinda 12, sare tatu na kufungwa mbili, akiibuka na ushindi mara tano kati ya zile sita za mwishoni mwa msimu.

Bryan Mbeumo aliyecheza mechi 34 na Benjamin Sesko (32), wamemaliza msimu wakiwa wafungaji bora wa kikosi cha Man United, kila mmoja akiwa ameingia kambani mara 12 kwenye mechi za mashindano yote.

Mbeumo’s 12 goals came in 34 appearances, while Sesko struck 12 in 32 matches, with the latter missing the end of the campaign due to a shin problem

Hata hivyo, hakuna anayestahili kuitwa Mchezaji Bora wa Mwaka wa klabu hiyo kama si kiungo raia wa Ureno, Bruno Fernandes.

Nyota huyo alichangia mabao 30 katika mechi 35, akiingia kambani mara tisa na kutoa ‘asisti’ 21 katika mechi 35 za michuano yote.

Kutokana na ubora wake huo, ndiye aliyetwaa tuzo kubwa mbili; Mchezaji Bora wa Mwaka wa Chama cha Waandishi wa Habari za Soka nchini England (FWA) na Mchezaji Bora wa Mwaka wa EPL.

Carrick (44), amepewa mkataba wa miaka miwili kuendelea kuliongoza benchi la ufundi. Je, atakuja na maajabu yapi msimu ujao?

Related articles

Recent articles