23.6 C
New York

Rooney: Nilitishiwa kuuawa kisa Man United

Published:

MANCHESTER, Uingereza

MPACHIKAJI mabao wa zamani wa Manchester United, Wayne Rooney, amefichua alivyowahi kupokea vitisho vya kuuawa baada ya kujiunga na klabu hiyo akitokea Everton.

Mwaka 2004, wakati huo akiwa na umri wa miaka 18, alikataa ofa nono ya kubaki Everton na kwenda Old Trafford kwa kitita cha Pauni milioni 27.

Kwa mujibu wa Rooney, uhamisho huo ulimsababishia uhasimu mkubwa mbele ya mashabiki wa Everton ya mjini Merseyside.

“Nilipokea vitisho vya kuuawa. Nyumba ya wazazi wangu ilichorwa jumbe. Ni kama ilivyokuwa kwa mpenzi wangu, ambaye sasa ni mke wangu,” anasema.

Manchester United ni mahasimu wakubwa wa mashabiki wa soka wa mjini Merseyside, ambako ndiko ziliko Everton na Liverpool.

“Kuondoka (Everton) ilikuwa ngumu kwa sababu nilikwenda Manchester United, ni kwa sababu Liverpool na Manchester United ni mahasimu wakubwa,” amesema.

Related articles

Recent articles