3.9 C
New York

Rais Samia azungumza na Kaimu Balozi wa Marekani

Published:

Na Mwandishi Wetu, Gazetini


RAIS  Samia Suluhu Hassan, amekutana na kuzungumza na Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Andrew Lentz, wakijikita katika  kudumisha ushirikiano wa kiuchumi, kisiasa, kijamii pamoja na miradi mbalimbali ya maendeleo inayofanywa kwa kushirikiana na Marekani.

Mazungumzo hayo  yamefanyika leo Desema 8, 2025, Ikulu Chamwino, mkoani Dodoma ambapo   pande zote mbili zimeeleza nia ya kuimarisha na kupanua ushirikiano kati ya mataifa hayo mawili.

Rais Samia amesisitiza umuhimu wa kuendeleza miradi ya maendeleo inayolenga kuinua uchumi wa wananchi na kuongeza fursa za ajira, huku Balozi Lentz akionyesha msukumo wa Marekani katika kushirikiana na Tanzania kwenye sekta mbalimbali za maendeleo.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img