8.4 C
New York

Nyasi zitawaka moto Afcon 2025: Kundi F

Published:

CAIRO, Misri
FAINALI za mwaka huu za Mataifa ya Afrika (AFCON 2025) zinatarajiwa kuanza kutimua vumbi lake Desemba 21, mwaka huu, na zitafikia ukomo Januari 18, mwakani.
Uchambuzi unaliangazia Kundi F, ambalo linazikutanisha Cameroon, Gabon, Ivory Coast na Msumbiji.
Cameroon ‘Indomitable Lions’ yenye mataji matano ndiyo timu ya pili (baada ya Misri) kwa mafanikio katika historia ya AFCON. Hii ni mara ya 22 kwao kushiriki.
Baada ya kushika nafasi ya tatu mwaka 2021, msimu uliopita wa mashindano hayo uliishuhudia Cameroon iliishia hatua ya 16 Bora.
Gabon, kwa upande wao, hii ni mara ya tisa kwa Taifa hilo kushiriki fainali za AFCON. Mafanikio makubwa zaidi kwao ni kufika robo fainali mara mbili (1996 na 2012).
Msimu uliopita, 2023, Gabon ilipiga hatua moja na kufika 16 Bora, ikiwa ni baada ya misimu miwili mfululizo ya kuishia hatua ya makundi.
Ivory Coast wataingia kwenye fainali hizo wakiwa ni mabingwa watetezi. Ni mara ya tatu kutwaa taji la AFCON. Pia, ni mara yao ya 26 kucheza michuano hiyo.
Ikumbukwe, kabla ya ubingwa wa mwaka 2023, Ivory Coast hawakuwahi kufika nusu fainali ya michuano ya AFCON tangu mwaka 2012.
Msumbiji ‘Mambas’ wamekuwa kwenye fainali hizo kwa misimu mitano. Hata hivyo, mara zote hizo waliishia hatua ya makundi kwenye mashindano hayo.
Kabla ya kushiriki mwaka 2023, Msumbiji walikuwa wamezikosa fainali hizo kwa miaka 13, tangu mwaka 2010.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img