8.4 C
New York

Nyasi zitawaka moto Afcon 2025: Kundi E

Published:

CAIRO, Misri
FAINALI za mwaka huu za Mataifa ya Afrika (AFCON 2025) zinatarajiwa kuanza kutimua vumbi lake Desemba 21, mwaka huu, na zitafikia ukomo Januari 18, mwakani.
Uchambuzi unaliangazia Kundi E, ambalo linazikutanisha Algeria, Burkina Faso, Guinea ya Ikweta na Sudan.
Algeria ‘Desert Foxes’ watakwenda Morocco wakifukuzia taji la la tatu la fainali za AFCON. Waliwahi kuwa mabingwa katika miaka ya 1990 na 2019. Hii ni mara yao ya 21 kushiriki mashindano hayo.
Chini ya kocha Vladimir Petkovic, kikosi hicho kina nyota kadhaa wanaocheza Ulaya, akiwamo Rayan Ait-Nouri wa Manchester City.
Kwa misimu miwili mfululizo, Algeria haijawa na mwenendo mzuri AFCON. Imeishia hatua ya makundi mara zote mbili, tangu ilipotwaa ubingwa wa mwisho.
Burkina Faso, kwa upande wao, hii ni mara yao ya 14 kuwa sehemu ya fainali hizo. Mafanikio makubwa zaidi kwao ni kufika fainali mwaka 2013, ambapo walifungwa na Nigeria.
Ni Burkina Faso yenye mastaa kadhaa, wakiwamo Dango Ouattara (Brentford), Issa Kabore (Manchester City) na Bertrand Traore (Sunderland).
Kama itakumbukwa, Burkina Faso walifika nusu fainali mwaka 2021 lakini safari yao msimu uliopita (2023) ilikwamia hatua ya 16 Bora.
Guinea ya Ikweta walishiriki kwa mara ya kwanza mwaka 2012, ambapo walikuwa wenyeji wa fainali hizo za AFCON wakishirikiana na Gabon.
Safari hii, watakwenda Morocco ikiwa ni mara yao ya tano kushiriki na mafanikio makubwa zaidi kwao ni kufika nusu fainali mwaka 2015.
Kwa misimu yote miwili iliyopita, 2021 na 2023, walivuka hatua ya makundi na kufika robo fainali na hatua ya 16 Bora.
Sudan, moja ya mataifa yaliyoasisi AFCON mwaka 1957, watashiriki fainali hizo kwa mara ya 10. Ni mabingwa mara moja na ilikuwa mwaka 1970.
Baada ya kufika robo fainali mwaka 2021, waliishia hatua ya makundi ya michuano hiyo msimu uliopita (2023).

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img