8.4 C
New York

Nyasi zitawaka moto Afcon 2025: Kundi B

Published:

CAIRO, Misri
FAINALI za mwaka huu za Mataifa ya Afrika (AFCON 2025) zinatarajiwa kuanza kutimua vumbi lake Desemba 21, mwaka huu, na zitafikia ukomo Januari 18, mwakani.
Uchambuzi unaliangazia Kundi B, ambalo linazikutanisha Angola, Misri, Afrika Kusini na Zimbabwe.
Angola ‘Black Sable Antelopes’, wanashiriki fainali za AFCON kwa msimu wao wa tisa na mafanikio makubwa zaidi kwao ni kufika hatua ya robo fainali mara tatu (2006, 2008 na 2010).
Hata hivyo, tangu walipogusa robo fainali mwaka 2010, Angola haijawahi kuvuka hatua ya makundi kwenye mashindano hayo makubwa zaidi barani Afrika.
Wakati huo huo, Misri ndiyo Taifa lenye mataji mengi zaidi (7) ya AFCON. Msimu huu ni wa 27 kwao kushiriki michuano hiyo.
Lakini, ‘Mafarao’ hawajawa mabingwa wa AFCON tangu mwaka 2010. Si tu ubingwa, bali pia hawajawahi kufika robo fainali ya mashindano hayo tangu kipindi hicho.
Kama kawaida, tegemeo lao katika michuano ya mwaka huu ni mshambuliaji wa Liverpool, Mohamed Salah, ingawa pia wanaye staa wa Manchester City, Omar Marmoush.
Afrika Kusini ‘Bafana Bafana’, licha ya utajiri wa vipaji vya soka, imetwaa mara moja pekee taji la AFCON na hiyo ilikuwa mwaka 1996.
Safari hii, wanakwenda kushiriki fainali hizo kwa msimu wa 12. Mafanikio yao makubwa kwa miaka ya hivi karibuni ni kushika nafasi ya tatu msimu uliopita, 2023.
Zimbabwe, kwa upande wao, watashiriki fainali za AFCON kwa mara ya sita. Walifanya hivyo katika miaka ya 2004, 2006, 2017, 2019 na 2021.
Baada ya kushindwa kufuzu msimu uliopita, 2023, Zimbabwe wanarejea AFCON lakini historia inatambua kuwa Taifa hilo halijawahi kuvuka hatua ya makundi.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img