8.4 C
New York

Nyasi zitawaka moto Afcon 2025: Kundi A

Published:

CAIRO, Misri
FAINALI za mwaka huu za Mataifa ya Afrika (AFCON 2025) zinatarajiwa kuanza kutimua vumbi lake Desemba 21, mwaka huu, na zitafikia ukomo Januari 18, mwakani.
Uchambuzi uaanza kwa kuliangazia Kundi A, ambalo linazikutanisha Morocco (wenyeji), Comoro, Mali na Zambia.
Morocco watashiriki AFCON kwa mara ya 20, ingawa ni mabingwa mara moja pekee, 1976, katika michuano hiyo ya Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF).
‘Simba wa Atlas’ wanaandaa fainali hizo kwa mara ya pili baada ya mwaka 1988, ambapo hata hivyo waliishia hatua ya nusu fainali.
Ni miaka mitatu pekee imepita tangu Morocco ilipoandika historia ya kuwa Taifa la kwanza la Afrika kufika nusu fainali ya Kombe la Dunia.
Mafanikio yao makubwa kwa misimu mitano ya hivi karibuni katika mashindano ya AFCON ni kufika mara mbili hatua ya robo fainali (2017 na 2021).
Kikosi chao kinaundwa na mastaa wengi wanaocheza soka la kulipwa barani Ulaya, wakiwamo ikiwamo Ligi Kuu ya England; Chadi Riad (Crystal Palace), Noussair Mazraoui (Manchester United) na Chemsdine Talbi (Sunderland).
Comoro waliishangaza Afrika walipofuzu kwa mara ya kwanza mwaka 2021 na kufika hatua ya 16 Bora ya michuano hiyo iliyofanyika nchini Cameroon.
Kwa upande wake, Mali watashiriki AFCON kwa mara ya 14. Mafanikio yao makubwa ni kufika fainali mwaka 1972, ambapo walifungwa na DRC iliyotwaa ubingwa huo.
Katika misimu mitatu ya hivi karibuni, Taifa hilo la Afrika Magharibi halijashindwa kuvuka hatua ya makundi ya AFCON. Msimu uliopita, 2023, Mali iliishia robo fainali.
Ni kikosi chenye uzoefu wa Ligi Kuu ya England kutokana na uwepo wa Cheick Doucoure (Crystal Palace), Yves Bissouma (Tottenham) na Boubacar Traore (Wolves).
Zambia ‘Chipolopolo’, waliishangaza Afrika walipotwaa ubingwa wa AFCON mwaka 2012. Haijavuka hatua ya makundi tangu ilipotwaa ubingwa huo.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img