19.5 C
New York

Rekodi zinazomsubiri Messi kabla ya kustaafu

Published:

MIAMI, Marekani
KUWEKA na kuvunja rekodi si jambo geni kwa Lionel Messi. Amefanya hivyo kwa miaka mingi, tangu akiwa Barcelona, hadi alipokuwa PSG, na sasa akiitumikia Inter Miami ya Ligi Kuu ya Marekani (MLS).
Hivi karibuni, Muargentina huyo alisaini mkataba mpya Inter Miami, hivyo atabaki klabuni hapo hadi mwaka 2028.
Je, ni rekodi zipi zinazomsubiri nahodha huyo wa timu ya taifa ya Argentina? Makala haya yanachambua. Endelea kusoma.
Nahodha wa Kombe la Dunia
Messi akiwa nahodha, Argentina walikuwa mabingwa wa Kombe la Dunia mwaka 2018. Katika historia ya michuano hiyo, hakuna mchezaji aliyewahi kutwaa ubingwa mara mbili akiwa nahodha.
Hivyo, Messi ataweka rekodi hiyo endapo ataiongoza Argentina yake kuwa mabingwa wa mashindano hayo yatakapofanyika hapo mwakani katika mataifa ya Marekani, Canada na Mexico.
Wachezaji waliowahi kutwaa ubingwa wa Kombe la Dunia mara moja wakiwa manahodha ni Giuseppe Meazza (Italia, 1938), Bellini (Brazil, 1958), Mauro (Brazil, 1962), Cafu (Brazil, 2002), na Daniel Passarella (Argentina, 1978).
Kinara wa ‘asisti’ duniani
Kwa mujibu wa rekodi zilizopo, mshambuliaji hatari wa zamani wa timu ya taifa ya Hungary, Ferenc Puskas, ndiye kinara wa pasi za mabao (asisti) duniani.
Hadi anastaafu, Puskas alikuwa na asisti 404, idadi ambayo Messi aliifikia siku chache zilizopita katika mchezo kati ya Inter Miami na Cincinnati.
Mabao ya faulo
Kwa sasa, Messi amewazidi David Beckham, Pele na Cristiano Ronaldo lakini anashika nafasi ya nne katika orodha ya wachezaji waliofunga mabao mengi ya aina hiyo.
Akiwa na mabao 69, mkali huyo amezidiwa na Juninho Pernambucano (72), Roberto Dinamite (75) na Marcelinho (78).
Kiatu cha ufungaji bora MLS
Msimu uliopita, alitwaa tuzo ya mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Marekani (MLS) akiwa amezifumania nyavu mara 29. Ni kiatu chake cha tisa tangu alipoanza kucheza soka.
Hata hivyo, hakuna mchezaji aliyewahi kutetea tuzo hiyo katika historia ya MLS. Kuibeba mara mbili mfululizo kutamfanya Messi kuvunja rekodi hiyo.
Mabao mengi zaidi MLS
Staa wa zamani wa Arsenal, Carlos Vela, ndiye mchezaji anayeshikilia rekodi ya kufunga mabao mengi ndani ya msimu mmoja wa MSL. Alifunga 34 akiwa na Los Angeles FC mwaka 2019.
Kama itakumbukwa, Messi alikaribia kuivunja rekodi hiyo lakini alikosa mabao sita pekee. Alimaliza msimu akiwa amezifumania nyavu mara 29.

Related articles

Recent articles