12.7 C
New York

Simulizi (2): Taribo West; Kutoka kutumia ‘hirizi’ uwanjani hadi uchungaji kanisani

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini
KATIKA ulimwengu wa soka, wachezaji wengi wanatufundisha kuhusu maadili, juhudi, na vipaji vya ajabu. Lakini kwa Taribo West, nyota wa zamani wa timu ya taifa ya Nigeria ‘Super Eagles’, ana simulizi ya kipekee.
Taribo alikuwa maarufu ulimwenguni kwa ustadi wake uwanjani, akicheza eneo la kiungo wa ulinzi na wakati mwingine beki wa kati akiwa na Eagles na klabu mbalimbali za Ulaya, ikiwamo Inter Milan.
Enzi zake uwanjani, mbali ya uwezo wake, Taribo alifahamika pia kwa namna alivyokuwa akiendekeza imani za kishirikina.
Mbali ya mazoezi, Taribo aliamini katika nguvu ya ‘hirizi’ aliyotembea nayo akiitegemea kumsaidia awapo uwanjani.
Aliamini hirizi za aina fulani zenye mwonekano wa pembe za mbuzi au nywele za wanyama wa porini zilikuwa zikiingia kwenye mchezo wake na kumsaidia kufanikiwa.
Ilitokea mara kadhaa katika mechi muhimu za Serie A akiwa na Inter Milan, kumuona Taribo akimshukuru Mungu kupitia hirizi. Hii ikisababisha wakati mwingine ataniwe na wachezaji wenzake.
Hata hivyo, maisha hayo ya soka yalipata mabadiliko makubwa baada ya Taribo kuachana na mchezo huo. Akawa ni Taribo wa tofauti, mwenye mabadiliko makubwa ya kiroho.
Alianza kujiuliza kuhusu maisha yake ya zamani, na hasa kuhusu imani za shirikina, na huo ukawa mwanzo wa ukurasa mpya. “Nilikuwa nikiishi kwa kutafuta nguvu kutoka kwa hirizi, lakini sasa ninapata nguvu kutoka kwa Mungu,” anasema.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img