10.2 C
New York

Kuelekea Kombe la Dunia: Ecuador (14)

Published:

QUITO, Ecuador
INASHIKA nafasi ya 23 katika viwango vya ubora vya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA). Mwaka 2013, Taifa hilo lilisogea hadi nafasi ya 10.
‘La Tricolor’ hawajawahi kuwa mabingwa wa michuano yoyote mikubwa na kwa sasa wako chini ya kocha Sebastian Beccacece, aliyeajiriwa tangu Agosti, mwaka jana.
Kocha huyo amekuwa na mafanikio makubwa kwenye ajira yake hiyo kwani amefungwa mechi moja pekee kati ya 16 alizokaa kwenye benchi la ufundi.
Miongoni mwa nyota tegemeo wa kikosi hicho ni Felix Torres na Gonzalo Plata wanaowika Ligi Kuu ya Brazil wakiwa na klabu za Corinthians na Flamengo.
Wakati huo huo, Enner Valencia aliyefunga mabao sita katika mechi za kufuzu ni miongoni mwa nyota wanaotarajiwa kuipaisha Ecuador msimu ujao wa Kombe la Dunia.
Msimu uliopita wa Kombe la Dunia, 2022, waliishia hatua ya makundi, ingawa walianza vizuri kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji Qatar. Ni Kundi lililokuwa na Uholanzi na Senegal.
Ecuador wamekata tiketi ya kushiriki fainali zijazo wakiwa wamekusanya pointi 32 katika mechi 18 na hii inakuwa mara yao ya tano kucheza michuano hiyo.
Hata hivyo, kati ya mara nne zilizopita, ni mara moja pekee waliyoweza kuvuka hatua ya makundi. Ni mwaka 2006, ambapo waliishia hatua ya 16 Bora wakiondoshwa na England kupitia kwa bao la faulo la David Beckham katika dakika ya 60.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img