10.2 C
New York

Kuelekea Kombe la Dunia 2026: Tunisia (15)

Published:

TUNIS, Tunisia
WAKONGWE wa Afrika ya Kaskazini, ambao wanashika nafasi ya 40 katika viwango vya soka duniani. Walikuwa nafasi ya 14 miaka saba iliyopita.
Tunisia ‘Eagles of Carthage’ watakumbukwa kuwa ni mabingwa mara moja wa fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON).
Trabelsi aliyekuwa nahodha wa kikosi wakati Tunisia iliposhiriki Kombe la Dunia mwaka 1998, ndiye kocha kwa sasa tangu alipotangazwa Februari, mwaka huu, na ni mara yake ya pili kuinoa timu hiyo.
Kwa kile walichokionesha katika hatua ya kufuzu, ambapo Tunisia ilishinda mechi tisa kati ya 10, pia ikiwa haijaruhusu nyavu zake kutikiswa.
Miongoni mwa nyota wanaowapa jeuri mashabiki wa timu ya taifa ya Tunisia ni Mohamed Ali Ben Romdhane (Al Ahly), Ellyes Skhiri (Eintracht Frankfurt) na Ali Abdi (Nice).
Ben Romdhane anayefanya vizuri katika soka la Afrika akiwa Ligi Kuu ya Misri, aliifungia Tunisia mabao manne wakati wa mechi za kufuzu fainali zijazo za Kombe la Dunia.
Tunisia ilikata tiketi ikiwa na mechi mbili mkononi na hii itakuwa ni mara yao ya saba kuwa sehemu ya michuano hiyo ya FIFA.
Licha ya ushiriki huo, haijawahi kuvuka hatua ya makundi. Msimu uliopita, 2022, waliifunga Ufaransa bao 1-0 lakini ilishindwa kuvuka katika kundi lililokuwa na timu zingine mbili, Australia na Denmark.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img