10.2 C
New York

Kuelekea Kombe la Dunia 2026: Senegal (13)

Published:

DAKAR, Senegal
IKIWA nafasi ya 19 katika viwango vya ubora vya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), Senegal iliwahi kuwa ya 17 mwaka jana.
Senegal ni mabingwa wa fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka 2021 na kwa sasa wako chini ya kocha mzawa, Pape Thiaw, ambaye aliajiriwa mwaka jana.
Kama itakumbukwa, Thiaw alicheza mechi moja (dhidi ya Denmark) wakati Senegal ilipofika robo fainali ya Kombe la Dunia mwaka 2002.
Mshambuliaji wa Al Nassr ya Saudi Arabia ndiye tegemeo zaidi, ingawa kikosi kinao mastaa wengine, wakiwamo Ismaila Sarr (Crystal Palace) na Boulaye Dia (Lazio).
Mane, mfungaji bora wa muda wote wa Senegal, aliingia kambani mara tano katika mechi za kufuzu fainali zijazo zitakazofanyika Marekani, Canada na Mexico.
Baada ya kuishia makundi mwaka 2018 nchini Urusi, Senegal walirudi kivingine na kufika hatua ya 16 Bora katika fainali zilizofuata (2022) nchini Qatar.
Hata hivyo, bado ‘Simba wa Teranga’ hawajaweza kurudia kile walichokifanya mwaka 2002, ambapo walifika robo fainali.
Ni mabingwa wa finali za Mataifa ya Afrika mwaka 2021, ingawa walishindwa kutetea ubingwa wao msimu uliopita (2023).

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img