10.2 C
New York

Kuelekea Kombe la Dunia 2026: Scotland (33)

Published:

GLASGOW, Scotland
MWAKA 2007, Scotland ilipanda kwenye viwango vya ubora wa soka duniani na kushika nafasi ya 13. Kwa sasa, iko nafasi ya 36.
Timu yake ya taifa haijawahi kutwaa taji lolote kubwa katika ulimwengu wa soka na inarejea Kombe la Dunia baada ya kuikosa michuano hiyo tangu mwaka 1998.
Kwa sasa, benchi la ufundi liko chini ya kocha Steve Clarke. Scotland ni miongoni mwa timu zilizodumu na kocha mmoja kwa muda mrefu kwani Clarke aliajiriwa Mei, 2019.
Kama zilivyo timu nyingi zitakazokwenda Kombe la Dunia, Scotland nayo inajivunia baadhi ya nyota wake wanaokipiga barani Ulaya.
Baadhi ya wachezaji hao ni Scott McTominay (Napoli), John McGinn (Aston Villa) na Andy Robertson (Liverpool).
Katika mechi za kufuzu, Che Adams, Ryan Christie na McTominay walionesha viwango bora, ambapo kila mmoja alifunga mabao mawili kuibeba timu hiyo.
Safari hii, Scotland walifuzu kushiriki fainali za mwakani baada ya ushindi dhidi ya Denmark katika mchezo wa mwisho.
Ikumbukwe, wanakwenda Kombe la Dunia kwa mara ya tisa lakini ni baada ya kushindwa mara sita katika mchakato wa kuwania tiketi.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img