10.2 C
New York

Kuelekea Kombe la Dunia 2026: Qatar (19)

Published:

DOHA, Qatar
TAIFA hilo la barani Asia linashika nafasi ya 51 katika viwango vya ubora wa soka duniani. Kabla ya kushuka, Qatar walikuwa nafasi ya 34 mwaka jana.
‘Maroon’ ni wenyeji wa Kombe la Dunia mwaka 2022 na ni mabingwa mara mbili wa Kombe la Asia, ambapo walifanya hivyo katika miaka 2019 na 2023.
Walipotwaa mwaka 2023, Qatar waliandika historia ya kuwa taifa la kwanza kutetea ubingwa wa michuano hiyo tangu Japan walipofanya hivyo mwaka 2004.
Kocha wa zamani wa Real Madrid, Wolves na timu ya taifa ya Hispania, Julen Lopetegui, ndiye anayeinoa Qatar kwa sasa. Aliajiriwa Mei, mwaka huu.
Katika kikosi chake, Mhispania huyo anawategemea zaidi Akram Afif (Al-Sadd), Hassan Al-Haydos (Al-Sadd) na Almoez Ali (Al-Duhail).
Ali alikuwa na mchango mkubwa katika mechi za kufuzu, ambapo aliifungia Qatar jumla ya mabao 12.
Hii ni mara ya kwanza kwa Qatar kufuzu (siyo kushiriki). Waliposhiriki mwaka 2022, hawakupitia mechi za kufuzu, wakipewa tiketi ya moja kwa moja wakiwa wenyeji.
Wakiwa wenyeji, waliishia hatua ya makundi kwa kupoteza mechi zote tatu walizokutana na Uholanzi, Senegal na Ecuador.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img