12.7 C
New York

Kuelekea Kombe la Dunia 2026: Paraguay (39)

Published:

ASUNCION, Paraguay
IFAHAMIKE kuwa Paraguay wanashika nafasi ya 39 katika viwango vya ubora vya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA). Walikuwa nafasi ya nane mwaka 2001.
‘La Albirroja’ ni mabingwa mara mbili wa michuano ya Copa America, wakiwa wamebeba taji hilo katika miaka ya 1953 na 1979.
Ni baada ya miaka 16 ya kushindwa kufuzu, timu ya taifa ya Paraguay imerejesha ushiriki wao kwenye fainali za Kombe la Dunia.
Mara yao ya mwisho kushiriki Kombe la Dunia ilikuwa mwaka 2010 nchini Afrika Kusini, ambapo walifika robo fainali kwa mara ya kwanza tangu walipoanza kucheza michuano hiyo.
Walitolewa kwa kufungwa bao 1-0 na Hispania na sasa kocha wao ni Gustavo Alfaro, ambaye aliajiriwa Agosti, mwaka jana.
Itakumbukwa, Muargentina huyo alikuwa kocha wa timu ya taifa ya Ecuador katika fainali zilizopita za mwaka 2022.
Mchezaji anayetazamwa zaidi kikosini ni staa wa Atlanta United, Miguel Almiron. Alikuwa na umri wa miaka 16 tu wakati Paraguay iliposhiriki kwa mara ya mwisho Kombe la Dunia mwaka 2010.
Mbali ya Almiron, wachezaji wengine bora katika kikosi hicho ni Antonio Sanabria aliyefunga mabao manne katika mechi za kufuzu na Angel Romero.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img