PANAMA CITY, Panama
NI mara ya pili kwao kushiriki Kombe la Dunia baada ya kufanya hivyo mwaka 2018. Panama iko nafasi ya 30 katika viwango vya ubora wa soka duniani.
‘Los Canaleros’, ambayo haijawahi kutwaa taji kubwa la soka, kwa sasa kikosi chake kinanolewa na Thomas Christiansen, aliyeajiriwa mwaka 2020.
Kocha huyo wa kimatafa wa Denmark, aliiwezesha Panama kufuzu fainali zijazo za Kombe la Dunia ikiwa haijapoteza mechi.
Kwa sasa, kikosi hicho kinajivunia uwezo mkubwa wa wachezaji wake wawili, Jose Fajardo na Jose Luis Rodriguez, ambao kila mmoja alifunga mabao matatu katika mechi za kufuzu.
Wakati huo huo, kikosi hicho kinamtegemea nyota anayefanya vizuri Ligi Kuu ya Ufaransa (Ligue 1) akiwa na Marseille, Amir Murillo.
Waliposhiriki kwa mara ya kwanza Kombe la Dunia mwaka 2018, Panama walikuwa kundi moja na England, Ubelgiji na Tunisia. Waliishia hatua hiyo ya makundi.
Published:


