11.2 C
New York

Kuelekea Kombe la Dunia 2026: New Zealand (36)

Published:

WELLINGTON, New Zealand
TAIFA hilo la Ulaya linashika nafasi ya 86 katika viwango vya ubora vya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).
‘All Whites’ watashiriki fainali za Kombe la Dunia kwa mara ya tatu baada ya kushindwa kukata tiketi katika miaka ya 2014, 2018 na 2022.
Mara yao ya mwisho kushiriki ilikuwa mwaka 2010 katika fainali zilizofanyika kwa mara ya kwanza barani Afrika, Afrika Kusini ikiwa mwenyeji.
New Zealand iliishia makundi lakini haikufungwa katika mechi zote tatu, na badala yake ilitoa sare na Paraguay, Slovakia na Italia.
Safari hii, kikosi hicho kinanolewa na kocha Darren Bazeley, ambaye aliajiriwa na kuanza majukumu yake Novemba, 2022.
Chris Wood ni miongoni mwa nyota tishio wa kikosi hicho. Nyota huyo wa Nottingham Forest, alifunga mabao tisa katika mechi za kufuzu Kombe la Dunia.
Mtihani alionao kocha Bazeley na vijana wake ni kupata ushindi wa kwanza katika michuano hiyo. Katika mechi sita, wamefungwa tatu na kutoa sare tatu.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img