CAIRO, Misri
MWAKA 2010, Misri ilikuwa nafasi ya tisa katika viwango vya ubora wa soka duniani lakini kwa sasa ni ya 34.
Maarufu pia kwa jina la ‘Mafarao’, ni mabingwa mara saba wa michuano ya fainali za Mataifa Afrika (AFCON).
Historia inawatambua kuwa ni mabingwa wa fainali hizo katika miaka ya 1957, 1959, 1986, 1998, 2006, 2008 na 2010.
Kwa sasa, kikosi hicho kinanolewa na mshambuliaji wake wa zamani, Hossam Hassan, ambaye aliajiriwa Februari, mwaka jana.
Ikumbukwe, Hassan alianza kikosini katika mechi zote tatu za makundi wakati Misri ilipocheza Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza mwaka 1990.
Licha ya kuwa na wachezaji wengi wanaocheza soka la kiwango cha juu, tegemeo lao kuelekea Kombe la Dunia lipo kwa Mohamed Salah.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa klabu za Chelsea na AS Roma, ambaye kwa sasa anakipiga Liverpool, alifunga mabao tisa kuiwezesha Misri kufuzu fainali zijazo.
Ukiliweka kando jina la Salah, kikosi cha Misri kinao pia Omar Marmoush (Man City) na Trezeguet (Al Ahly).
Misri wanakwenda Kombe la Dunia kwa mara ya pili tangu walioishia hatua ya makundi ya mashindano hayo mwaka 2018. Ni Kundi lililokuwa na Urusi, Uruguay na Saudi Arabia.
Published:


