MEXICO CITY, Mexico
MWAKA 2006, Mexico ilikuwa katika nafasi ya nne kwenye viwango vya ubora wa soka vya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA). Kwa sasa ni ya 15.
Mexico ni miongoni mwa mataifa yenye mafanikio makubwa ya soka kwa upande wa CONCACAF, ikiwa na mataji 13 ya michuano ya Shirikisho hilo.
Rekodi zinaonesha kuwa ni mabingwa wa CONCACAF katika miaka ya 1965, 1971, 1977, 1993, 1996, 1998, 2003, 2009, 2011, 2015, 2019, 2023 na 2025.
Mabingwa hao wa Kombe la Mabara mwaka 1999 wako chini ya kocha Javier Aguirre, ambaye aliajiriwa mwaka jana na hii ni mara yake ya tatu kufanya kazi kwenye benchi la ufundi.
Kabla ya kurejea mwaka jana, Aguirre alikuwa kwenye benchi wakati Mexico ilipofika 16 Bora katika fainali za mwaka 2002 na 2010.
Mexico ina kikosi chenye mastaa kama Raul Jimenez (Fulham), Hirving Lozano (San Diego FC) na Guillermo Ochoa (AEL Limassol).
Wanashiriki kwa mara ya tisa mfululizo fainali hizi za Kombe la Dunia na waliishia hatua ya makundi msimu uliopita (2022).
Licha ya kuingia 16 Bora mara saba, Mexico haijawahi kushinda mechi yoyote ya hatua hiyo tangu walipofika robo fainali wakiwa wenyeji mwaka 1986.
Published:


