10.2 C
New York

Kuelekea Kombe la Dunia 2026: Jordan (18)

Published:

AMMAN, Jordan
TIMU ya taifa ya Jordan inashika nafasi ya 66 katika viwango vya ubora vya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA). Ni kutoka nafasi ya 37 mwaka 2004.
Jordan haijawahi kutwaa taji lolote kubwa na hii inakuwa mara ya kwanza kufuzu fainali za Kombe la Dunia.
Kocha ni Jamal Sellami, ambaye alianza kuinoa timu hiyo Agosti, mwaka jana. Ni mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Morocco.
Sellami alicheza mechi moja wakati wa fainali za Kombe la Dunia mwaka 1998. Alitokea benchi katika ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Scotland.
Miongoni mwa wachezaji tegemeo kikosini ni Ali Olwan (Al-Karma), Yazan Al Naimat (Al Arabi) na Musa Al Taamari (Rennes).
Olwan alikuwa mchezaji muhimu zaidi katika kufuzu, ambapo alifunga mabao tisa, ikiwamo ‘hat-trick’ iliyowahakikishia nafasi walipopata ushindi dhidi ya Oman.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img