10.2 C
New York

Kuelekea Kombe la Dunia 2026: Iran (17)

Published:

TEHRAN, Iran
TIMU ya soka ya taifa ya Iran iko nafasi ya 20 katika viwango vya ubora duniani. Walikuwa ya 15 mwaka 2005.
‘Team Melli’ ni mabingwa mara tatu wa Kombe la Asia. Walitwaa taji hilo katika miaka ya 1968, 1972 na 1976.
Kocha ni Amir Ghalenoei, ambaye aliajiriwa mwaka 2023, ikiwa ni mara yake ya pili kuliongoza benchi la ufundi la timu hiyo.
Ghalenoei aliwahi kuinoa timu hiyo msimu wa 2006-07 lakini alifungashiwa virago baada ya kufanya vibaya Kombe la Asia.
Katika mechi za kufuzu Kombe la Dunia, nyota aliyekuwa na mchango mkubwa zaidi ni Mehdi Taremi. Alifunga mabao 10.
Mbali ya Taremi anayecheza soka barani Ulaya katika klabu ya Olympiacos, mastaa wengine kkikosini ni Alireza Jahanbakhsh na Sardar Azmoun.
Iran watashiriki Kombe la Dunia kwa mara ya saba. Ni mara yao ya nne mfululizo kufuzu fainali hizo, ingawa hawajawahi kuvuka makundi.
Katika mechi 18 za Kombe la Dunia, Iran imeshinda tatu pekee, ikizifunga Wales (2022), Morocco (2018) na Marekani (1998).
Msimu uliopita, 2022, walishindwa kuingia hatua ya 16 Bora wakiwa Kundi moja na England, Marekani na Wales.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img