12.7 C
New York

Kuelekea Kombe la Dunia 2026: Hispania (34)

Published:

MADRID, Hispania
TAIFA linaloshika nafasi ya kwanza katika viwango vya ubora wa soka duniani. Timu yao ya taifa pia inafahamika kwa jina la ‘La Furia Roja’.
Hispania ni mabingwa mara moja wa Kombe la Dunia. Kama itakumbukwa, walitwaa taji hilo wakati wa michuano ya mwaka 2010 iliyofanyika Afrika Kusini.
Ifahamike pia, Hispania wamelibeba mara nne taji la fainali za Mataifa ya Ulaya (EURO), ambapo walifanya hivyo katika miaka ya 1964, 2008, 2012 na 2024.
Hispania, ambayo imeishia hatua ya 16 Bora mara mbili mfululizo katika fainali za Kombe la Dunia, kwa sasa inanolewa na Luis de la Fuente, ambaye aliajiriwa Desemba, 2022.
De la Fuente aliyekuwa kocha wa U-21 ya Hispania, ndiye aliyeipa mataji ya Ligi ya Mataifa ya Ulaya (Nations League) mwaka 2023 na fainali za Mataifa ya Ulaya (EURO) mwaka jana.
Katika mechi za kufuzu fainali zijazo za Kombe la Dunia, nyota waliokuwa moto zaidi ni Mikel Merino na Mikel Oyarzabal, ambao kila mmoja alifunga mabao sita.
Hata hivyo, mastaa wengine wanaotarajiwa kuipaisha Hispania hapo mwakani ni Lamine Yamal na Ferran Torres (Barcelona) na Rodri (Manchester City).
Kwa mujibu wa historia, mwakani itakuwa ni mara ya 17 kwa Hispania kushiriki fainali za Kombe la Dunia.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img