10.2 C
New York

Kuelekea Kombe la Dunia 2026: Haiti (23)

Published:

PORT-AU-PRINCE, Haiti
KWA mujibu wa viwango vya ubora wa soka duniani, Taifa hilo la Amerika ya Kaskazini linashika nafasi ya 84. Haiti iliwahi kusogea hadi nafasi ya 38 mwaka 2013.
‘Les Grenadiers’ ni mabingwa mara moja wa Kombe la CONCACAF, ambapo walitwaa taji hilo mwaka 1973.
Kwa sasa, kikosi kinanolewa na kocha Sebastien Migne, ambaye aliajiriwa Mei, mwaka jana. Alikuwa msaidizi wa Rigobert Song wakati Cameroon iliposhiriki Kombe la Dunia mwaka 2022 na fainali za AFCON mwaka jana.
Wana kikosi chenye baadhi ya mastaa wanaofanya vizuri barani Ulaya, wakiwamo Jean-Ricner Bellagarde (Wolves) na Frantzdy Pierrot (AEK Athens).
Wakati huo huo, mashabiki wa timu hiyo wanajivunia kiwango bora cha Duckens Nazon, ambaye alifunga mabao sita katika mechi za kufuzu.
Hii ni mara ya pili kwa Haiti kukata tiketi ya kushiriki fainali za Kombe la Dunia tangu mwaka 1974, ambapo walipoteza mechi zote tatu.
Kocha wao, Migne, hajawahi kwenda Haiti, hiyo ikitokana na hali mbaya ya usalama inayoendelea katika nchi hiyo.
Haiti wamekuwa wakifanya mazoezi na kucheza mechi zao za nyumbani katika nchi jirani za Barbados, Aruba na Curacao.
Safari hii, Haiti wanarejea Kombe la Dunia baada ya kushiriki fainali hizo mwaka 1974, ambapo waliishia makundi katika Kundi lililokuwa na Poland, Argentina na Italia.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img