WILLEMSTAD, Curacao
VIWANGO vya ubora vya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) linaionesha Curacao ikiwa nafasi ya 82 duniani. Iliwahi kufika nafasi ya 68 mwaka 2017.
‘Blue Family’ wako chini ya kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Uholanzi, Dick Advocaat, ambaye aliajiriwa Januari, mwaka jana.
Advocaat aliyekuwa kocha wa Uholanzi katika fainali za Kombe la Dunia za mwaka 1994, pia aliiongoza Korea ya Kusini mwaka 2006.
Katika fainali zijazo, Mholanzi huyo mwenye umri wa miaka 78 atakuwa kocha mzee zaidi kushiriki michuano hiyo ya FIFA.
Kwamba atakuwa ameipiku rekodi ya Otto Rehhagel, ambaye alikuwa kocha wa Ugiriki akiwa na miaka 71 mwaka 2010.
Katika mechi za kuwania tiketi ya kushiriki fainali za Kombe la Dunia za mwakani, mshambuliaji wao, Gervane Kastaneer, ndiye aliyeibeba Curacao kwa mabao yake matano.
Nyota wengine temegeo kwenye mipango ya kocha Advocaat ni Leandro Bacuna (Bandimarspor), Juninho Bacuna (Gaziantep) na Gervane Kastaneer.
Kisiwa hicho cha Caribbean kina watu 150,000 na kinaandika historia ya kuwa Taifa dogo zaidi kuwahi kufuzu Kombe la Dunia.
Kutokana na ukaribu wake mkubwa na Uholanzi, asilimia kubwa ya wachezaji wake walizaliwa katika nchi hiyo ya Ulaya.
Published:


