11.2 C
New York

Kuelekea Kombe la Dunia 2026: Colombia (38)

Published:

BOGOTA, Colombia
NAFASI ya 13 katika viwango vya ubora wa soka duniani. Mwaka 2016, Colombia ilipiga hatua kubwa zaidi kwa kushika nafasi ya tatu.
‘La Tricolor’ ni mabingwa mara moja kwa upande wa michuano ya Copa America na walifanya hivyo mwaka 2001.
Hii inakuwa mara ya saba kwao kufuzu Kombe la Dunia, ingawa walizikosa fainali zilizopita za mwaka 2022 zilizofanyika nchini Qatar.
Kwa sasa, kikosi chao kinanolewa na mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Argentina, Nestor Lorenzo, aliyeajiriwa mwaka 2022.
Nahodha wa kikosi ni kiungo wa zamani wa Real Madrid, James Rodriguez, ambaye aliwika katika fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2014.
Katika michuano hiyo, nyota huyo mwenye umri wa miaka 34 kwa sasa aliibuka mfungaji bora akiwa amezipasia nyavu mara sita na kuiwezesha Colombia kufika robo fainali.
Safari hii, ikiwa ni mara yao ya saba kucheza Kombe la Dunia, Colombia wana kikosi chenye mastaa wengi, wakiwamo Luiz Diaz (Bayern Munich), Rodriguez (Leon) na Richard Rios (Benfica).
Diaz aliyejiunga na Bayern majira haya ya kiangazi akitokea Liverpool, alichangia Colombia kufuzu fainali zijazo za Kombe la Dunia baada ya kufunga mabao saba.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img