TORONTO, Canada
NI baada ya ushindi dhidi ya Panama, ndipo timu ya soka ya taifa ya Canada ilipojihakikishia nafasi ya kushiriki fainali zijazo za Kombe la Dunia.
Canada, maarufu pia kwa jina la ‘The Reds’, wanashika nafasi ya 27 katika viwango vya ubora vya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).
Kwa sasa, kikosi hicho kinanolewa na kocha aliyewahi kufanya kazi Ligi Kuu ya England akiwa na Southampton, Jesse Marsch, aliyeajiriwa Mei, mwaka jana.
Marsch alianza vibaya kibarua chake baada ya kufungwa mabao 4-0 na Uholanzi. Mechi iliyofuata, alipata suluhu dhidi ya Ufaransa, kabla ya kuiongoza Canada kushika nafasi ya nne katika michuano ya Copa America.
Kuelekea fainali hizo za mwakani, Canada inajivunia kikosi chenye wachezaji wanaotamba na klabu kubwa za Ulaya, wakiwamo Jonathan David (Juventus), Cyle Larin (Feyenoord) na Alphonso Davies (Bayern Munich).
Baada ya miaka 36 ya kukosa ushiriki wa Kombe la Dunia, walirejea kwenye michuano hiyo mwaka 2022.
Hata hivyo, Canada waliishia hatua ya makundi nchini Qatar baada ya kupoteza mechi zote tatu dhidi ya Ubelgiji, Morocco na Croatia.
Davies alifunga bao lao pekee kwenye historia ya Kombe la Dunia katika mchezo ambao hata hivyo walikutana na Croatia na kufungwa mabao 4-1.
Marsch, ambaye pia aliwahi kufanya vizuri Ligi Kuu ya Ujerumani (Bundesliga), Canada ilifuzu ikiwa kwenye Kundi lililokuwa pia na Uholanzi.
Published:


