12.7 C
New York

Kuelekea Kombe la Dunia 2026: Brazil (37)

Published:

RIO, Brazil
NAFASI ya tano katika viwango vya ubora wa soka duniani. Brazil waliwahi kushika nafasi ya kwanza mwaka 2023.
Brazil, maarufu kwa jina la ‘Selecao’ au ‘Canarinho’, ni mabingwa mara tano wa Kombe la Dunia; 1958, 1962, 1970, 1994 na 2002.
Pia, timu ya taifa ya Brazil imebeba mara tisa taji la Copa America, ikifanya hivyo katika miaka ya 1919, 1922, 1949, 1989, 1997, 1999, 2004, 2007 na 2019.
Carlo Ancelotti aliyeajiriwa Mei, mwaka huu, hii ni mara yake ya kwanza kupewa majukumu ya kunoa timu ya taifa. Ni mara yake ya kwanza pia kufanya kazi nje ya Ulaya.
Muitalia huyo ana mataji makubwa 23 katika maisha yake ya ufundishaji soka, yakiwamo matano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Katika mechi za kufuzu, Raphinha wa Barcelona aliifungia Brazil jumla ya mabao matano lakini pia kikosi chao kina mastaa wengi, wakiwamo Vinicius Junior (Real Madrid) na Estevao (Chelsea).
Hata hivyo, mtihani walionao ni kuifikisha Brazil katika hatua ya fainali kwani haijafika tangu ilipotwaa ubingwa mwaka 2002.
Ikumbukwe, Brazil iliishia robo fainali msimu uliopita wa Kombe la Dunia, ambapo walitolewa na Croatia kwa mikwaju ya penalti.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img