CANBERRA, Australia
TIMU ya soka ya taifa ya Australia inashika nafasi ya 26 katika viwango vya ubora duniani. Iliwahi kuwa ya 14 mwaka 2009.
‘Socceroos’ watashiriki kwa mara ya sita mfululizo fainali za Kombe la Dunia. Waliishia hatua ya 16 Bora msimu uliopita.
Katika fainali hizo zilizofanyika Qatar, walivuka makundi kwa kuifunga Denmark bao 1-0 lakini waliondoshwa na Argentina kwa kipigo cha mabao 2-1.
Australia iko chini ya kocha mpya, Tony Popovic, ambaye alianza majukumu ya kukinoa kikosi hicho Septemba, mwaka jana.
Popovic ni mchezaji wa zamani wa timu hiyo na alicheza mechi moja wakati wa fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2006.
Je, wanakwenda kuandika historia ya kuingia kwa mara ya kwanza hatua ya robo fainali ya michuano hiyo ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA)?
Published:


