ALGIERS, Algeria
KATIKA viwango vya ubora vya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), vigogo hao wa Kaskazini mwa Afrika wako nafasi ya 35. Waliwahi kufika ya 15 mwaka 2014.
Maarufu pia kwa jina la ‘The Greens’, Algeria ni mabingwa mara mbili wa fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON); 1990 na 2019.
Kwa sasa kocha ni Vladimir Petkovic, ambaye amekuwa kwenye benchi la ufundi tangu Februari, mwaka jana.
Raia huyo wa Bosnia ni kocha mwenye uzoefu mkubwa kwenye michuano hiyo ya Kombe la Dunia, akikumbukwa kwa kuifikisha Uswis katika hatua ya 16 Bora mwaka 2018.
Katika hatua ya kufuzu, staa aliyekuwa na mchango mkubwa zaidi ni Mohamed Amoura. Nyota huyo wa Wolfsburg ya Bundesliga alifunga mabao 10.
Kwa upande mwingine, Morocco wanakwenda Kombe la Dunia wakiwa na kikosi chenye mastaa wengi, wakiwamo Riyad Mahrez (Al AhIi) na Rayan Ait-Nouri (Man City).
Algeria wamerejea Kombe la Dunia baada ya misimu miwili ya kukosekana kwenye michuano hiyo. Mara ya mwisho, walifika hatua ya 16 Bora wakitolewa na Ujerumani kwa kichapo cha mabao 2-1.
Je, Algeria watakaoshiriki Kombe la Dunia kwa mara ya tano, wataandika historia ya kufika robo fainali kwa mara ya kwanza?
Published:


