LONDON, Uingereza
ARGENTINA inashika nafasi ya pili katika viwango vya ubora wa soka dunaini. Imeporomoka kwa nafasi moja kwani ilikuwa ya kwanza Julai, mwaka huu.
‘La Albiceleste’ ni mabingwa mara tatu wa fainali za Kombe la Dunia. Walitwaa ubingwa huo katika miaka ya 1978, 1986 na 2022.
Pia, Taifa hilo la Amerika ya Kusini ni mabingwa wa Copa America mara nyingi zaidi (16); 1921, 1925, 1927, 1929, 1937, 1941, 1945, 1946, 1947, 1955, 1957, 1959, 1991, 1993, 2021 na 2024.
Kocha wao kwa sasa ni Lionel Scaloni, ambaye amekuwa kwenye benchi la ufundi la timu hiyo tangu Agosti, 2018.
Argentina Ina kikosi kilichojaza mastaa wakubwa wa soka, ikitosha kuwataja Lionel Messi (Inter Miami), Lautaro Martinez (Inter Milan) na Julian Alvarez (Atletico Madrid).
Katika harakati za kutafuta tiketi ya kushiriki fainali zijazo za Kombe la Dunia, Messi alikuwa na msaada mkubwa baada ya kufunga mabao nane.
Watakwenda katika fainali hizo wakiwa Mabingwa watetezi. Mwaka 2022, Messi alikuwa nahodha wa kwanza kutwaa taji hilo tangu Diego Maradona alipofanya hivyo mwaka 1986.
Baada ya mafanikio hayo, Argentina walinyakua Copa America mwaka jana na hii inakuwa mara yao ya 18 kushiriki Kombe la Dunia.
Published:


