10.9 C
New York

Mastaa 12 hawa ‘out’ Kombe la Dunia 2026

Published:

LONDON, Uingereza
FAINALI za Kombe la Dunia za mwakani ziko njiani, ikiwa ni kwa mara ya kwanza michuano hiyo itashuhudia timu 48 zikishiriki.
Miongoni mwa timu kubwa zilizokata tiketi ni England, Argentina, Brazil, Ufaransa na Ureno, lakini fainali hizo zitawakosa baadhi ya mastaa kutokana na mataifa yao kushindwa kufuzu.
Benjamin Sesko (Slovenia)
Straika wa Manchester United, ambaye usajili wake kutoka RB Leipzig ya Bundesliga uligharimu kitita cha Pauni milioni 47.
Sesko hatokwenda Kombe la Dunia baada ya timu yake ya taifa ya Slovenia kushindwa kukata tiketi ikiwa imekosa ushindi katika mechi zote tano.
Onana & Mbeumo (Cameroon)
Nyota wawili wa timu ya taifa ya Cameroon, Andre Onana na Bryan Mbeumo, nao watabaki nyumbani baada ya Taifa lao kushindwa kufuzu fainali hizo.
Cameroon iliingia ‘play-off’ lakini ilifungwa na DRC itakayoiwakilisha Afrika katika mchujo wa mwisho wa kuamua timu moja itakayokwenda Kombe la Dunia.
Szoboszlai & Kerkez (Hungary)
Mastaa wawili hao, Dominik Szoboszlai na Milos Kerkez, pia watabaki kuwa washangiliaji wakati wa fainali zijazo za Kombe la Dunia huko Marekani, Canada na Mexico.
Timu yao ya taifa ya Hungary ilikaribia kuingia hatua ya playoff, kabla ya kufungwa na Jamhuri ya Ireland katika mchezo wa mwisho.
Osimhen, Iwobi & Lookman
Baada ya timu ya taifa ya Nigeria kutokufuzu, fainali za Kombe la Dunia hazitawashuhudia Victor Osimhen, Alex Iwobi na Ademola Lookman wakiwa uwanjani.
Nigeria, ambayo pia ilizikosa fainali zilizopita za mwaka 2022, ilifika hatua ya playoff lakini iliondoshwa na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).
Aubameyang & Lamina
Baada ya timu yao ya taifa ya Gabon kukosa nafasi, mastaa Pierre-Emerick Aubameyang na Mario Lamina watazikosa fainali hizo za Kombe la Dunia.
Gabon haijawahi kushiriki fainali hizo na safari hii ilikaribia kufuzu lakini ilipoteza matumaini baada ya kufungwa na Nigeria mabao 3-1.
Vlahovic & Mitrovic
Serbia kutoshiriki ni pigo kwa mastaa wake, Dusan Vlahovic na Aleksandar Mitrovic. Kama itakumbukwa, Serbia ilikuwa Kundi moja na England ‘Three Lions’.
Licha ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Latvia katika mchezo wa mwisho, Serbia ilizidiwa pointi moja tu na Albania iliyoshika nafasi ya pili.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img