14 C
New York

United imejipata au bado inajitafuta?

Published:

MANCHESTER, Uingereza
MANCHESTER United chini ya kocha Ruben Amorim iliuanza vibaya msimu huu wa Ligi Kuu ya England (EPL).
Kati ya mechi sita za mwanzo, ilishinda mbili pekee, ilifungwa tatu na kuambulia sare moja. Mambo yalikuwa magumu.
Hata hivyo, ni kama upepo umebadilika. Licha ya kwamba iko nafasi ya saba kwenye msimamo, Man United haijafungwa katika mechi zote tano za EPL ilizocheza hivi karibuni.
Baada ya kila timu kucheza mechi 11 na sasa ziko kwenye mapumziko ya kupisha kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), Man United imezidiwa pointi moja tu na Sunderland inayoshika nafasi ya nne.
Amorim, licha ya kutokuwahi kushinda mara mbili mfululizo kwenye Ligi tangu aajiriwe, alishinda mechi zote tatu za Oktoba, ambapo alikutana na Sunderland, Liverpool na Brighton.
Wakati huo huo, bado kocha Amorim ana kazi kubwa kwani Man United inaongoza kwa kuruhusu mabao ya kipindi cha pili msimu huu.
Kwa mujibu wa takwimu, Man United iliyomaliza katika nafasi ya 15 msimu uliopita, imeruhusu mabao 14 ya kipindi cha pili na imefunga nane pekee.
Lakini, akizungumza baada ya sare ya mabao 2-2 katika mchezo uliopita, Amorim aliyeajiriwa Old Trafford baada ya kazi nzuri aliyoifanya Sporting Lisbon, amesema:
“Naelewa kwamba hiki kinachotokea ni dalili tu ya mwanzo mzuri unaokuja. Bado tupo mwanzo wa kurejea kwenye ubora, tuna kazi kubwa ya kufanya.”
Kocha huyo raia wa Ureno anafahamu kuwa ameshinda mechi 12 pekee kati ya 38 za Ligi Kuu alizoiongoza Man United.
Wastani wake wa asilimia 31.6 ya ushindi wa mechi ni mdogo kuliko kocha yeyote aliyewahi kuajiriwa klabuni hapo.
Takwimu zinaonesha kuwa hata mtangulizi wake, Erik ten Hag, alikuwa bora zaidi kwani wastani wa ushindi wa mechi ulikuwa ni asilimia 51.8.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img