13.8 C
New York

Yanga yaizima KMC, yaing’oa Simba kileleni

Published:

Na Hassan Mwasha, Gazeini
HATIMAYE ushindi mnono wa mabao 4-1 dhidi ya KMC umeirejesha Yanga kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Matokeo hayo yamaeifanya ‘Timu ya Wananchi’ kukaa juu ikiwa na pointi 10 baada ya kushuka dimbani mara nne msimu huu wa 2025-26.
Yanga waliingia katika Uwanja wa KMC wakifahamu kuwa ushindi ungewatoa Simba kileleni, ambapo walikuwa wakiongoza wakiwa na pointi tisa.
Katika mchezo dhidi ya KMC, Yanga walianza kuziona nyavu za wapinzani hao dakika ya 37, mfungaji akiwa ni winga raia wa DRC, Max Nzengeli, ambaye alitumia ‘asisti’ ya Pacome Zouzoua.
Zikiwa zimebaki dakika mbili kumalizika kwa kipindi cha kwanza, KMC walisawazisha kupitia kwa Saliboko, hivyo timu hizo kwenda mapumziko zikiwa sare ya bao 1–1.
Dakika ya 73, Zouzoua aliwanyanyua vitini mashabiki wa Yanga na kuufanya ubao wa matokeo usomeke 2–1.
Yanga waliendeleza makali yao kwa KMC katika dakika ya 82, safari hii mfungaji wa bao akiwa ni Andy Boyeli aliyetokea benchi, ambaye pia ndiye aliyefunga bao la mwisho.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img