20.3 C
New York

Kocha Stars: Pointi nne zinatosha AFCON

Published:

Na Hassan Mwasha, Gazetini
KOCHA wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Hemed Suleiman, amesema pointi nne zinatosha kukivusha kikosi hicho hatua ya makundi ya fainali za Mataifa Afrika (AFCON) za mwaka huu nchini Morocco.
Huku michuano hiyo ikitarajiwa kuanza Desemba 21 na kumalizika Januari 18, mwakani, Stars imepangwa Kundi C, ambalo linazijumuhisha pia Nigeria, Uganda na Tunisia.
Akizungumzia ushindani huo, Hemed ‘Morocco’ amesema: “Tunajitaji walau pointi nne, hizo zitatufanya tuwe kwenye nafasi ya kwenda hatua ya mtoano. Ulinzi ndiyo jambo la msingi zaidi, kutokuruhusu bao ndiyo msingi wa mafanikio.”
Wakati huo huo, amesisitiza kuwa ili kufanya vizuri, lazima safu yake ya ushambuliaji nayo iwe kwenye makali ya kutumia kila nafasi inayopatikana.
“Kwa ushambuliaji, tunataka tuwe tunafunga kwa kila nafasi tunayopata …” amesema Morocco na kusisitiza kuwa nidhamu ya wachezaji ndani ya uwanja nayo ina nafasi kubwa.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img