24.8 C
New York

Aliyetaka kuinunua Everton akwaa kesi ya ufisadi

Published:

LONDON, Uingereza
MMOJA ya wamiliki wa kampuni ya uwekezaji ya 777 Partners, ambayo ilijaribu bila mafanikio kuinunua klabu ya Everton, anakabiliwa na mashitaka ya ufisadi.
Josh Wander mwenye umri wa miaka 44, anatajwa kughushi nyaraka za masuala ya fedha na kuiingizia kampuni yake hiyo kiasi cha Pauni milioni 372.
Kwa mujibu wa waendesha mashitaka wa Marekani, alitumia nyaraka hizo kuwaingiza ‘chaka’ wawekezaji mbalimbali.
“Wander alitumia nyaraka feki kudanganya wawekezaji wengine kuwa anamiliki baadhi ya vitu, ambayo si kweli kwamba kampuni yake inavyo.
“Hiyo ni pamoja na kughushi nyaraka za benki, pia akitengeneza baadhi ya nyaraka kudanganya juu ya masuala ya fedha ya kampuni yake,” amesema mmoja ya waendesha mashitaka hao, Jay Clayton.
Kupitia kampuni ya 777, bilionea Wander alitaka kuinunua Everton mwaka jana lakini mmliki wa klabu hiyo, Farhad Moshiri, aliiuza kwa Friedkin Group.

Related articles

Recent articles