24.8 C
New York

Afrika na safari ya Kombe la Dunia 2026 (8) – Ivory Coast

Published:

Na Hassan Mwasha, Gazetini
MATAIFA tisa ya Afrika yameshajihakikishia tiketi ya kushiriki fainali zijazo za Kombe la Dunia za mwakani zitakazofanyika Marekani, Canada na Mexico. Tunisia, Algeria, Ghana, Senegal, Misri, Afrika Kusini, Ivory Coast, Cape Verde na Morocco.
Makala haya yanawaangazia wawakilishi hao wa soka la Afrika kwa kuichambua Ivory Coast. Je, ina nafasi ya kufanya vizuri Kombe la Dunia?
Kuelekea mchezo wao wa mwisho wa kufuzu, Ivory Coast walikuwa kileleni mwa Kundi lao wakiizidi pointi mbili Gabon iliyokuwa nafasi ya pili.
Ivory Coast ‘The Elephants’ walicheza na Kenya na kuifunga mabao 3-0, wafungaji wakiwa ni nahodha Franck Kessie, Yan Diomande na Amad Diallo.
Vigogo hao wa soka la Afrika Magharibi walikaa kileleni mwa Kundi F wakiwa na pointi 26 na wanarejea Kombe la Dunia baada ya kuikosa michuano hiyo tangu mwaka 2014.
Katika mechi 10 za safari yao ya kuwania tiketi, Ivory Coast ilifunga mabao 25, huku safu yake ya ulinzi ikionesha kiwango bora cha kutokuruhusu nyavu zake kutikiswa.
Kikosi hicho kinanolewa na kocha mzawa, Fae. Ni kiungo wa zamni wa Ivory Coast na aliajiriwa mwaka jana kuchukua nafasi ya Jean-Louis Gasse aliyefukuzwa baada ya timu hiyo kuanza vibaya katika michuano ya AFCON.
Faye anakuwa kocha mzawa wa kwanza kuipa Ivory Coast tiketi ya kushiriki Kombe la Dunia. Je, pia atakuwa wa kwanza kupeleka timu hiyo hatua ya 16 bora?
Tujikumbushe; hii inakuwa mara ya nne kwa Taifa hilo lenye uchumi mkubwa barani Afrika kushiriki Kombe la Dunia lakini halijawahi kuvuka hatua ya makundi.
Je, watatimiza ndoto hiyo kupitia michuano ya mwakani huko Marekani, Canada na Mexico? “Hatupaswi kuridhika, bado kuna safari ndefu inayoanza baada ya kufuzu. Lazima tujitoea vya kutosha ndani ya uwanja,” amesema kocha Faye.

Related articles

Recent articles