24.8 C
New York

Ronaldo kinara wa mabao kufuzu Kombe la Dunia

Published:

LISBON, Ureno
BAADA ya kufunga mabao mawili jana, Cristiano Ronaldo amekuwa mchezaji aliyepasia nyavu mara nyingi katika historia ya mechi za kufuzu fainali za Kombe la Dunia.
Ronaldo mwenye umri wa miaka 40, amefikisha mabao 41 akimpiku Carlos Ruiz (39) aliyekuwa akishikilia rekodi hiyo.
Katika mchezo wa jana, Ureno ikiwa nyumbani mjini Lisbon ililazimishwa sare ya mabao 2-2 na Hungary, hivyo kushindwa kufuzu.
Ni kwa maana hiyo basi, ili Ureno kufuzu, italazimika kuifunga
Jamhuri ya Ireland katika mchezo wa ugenini wa Novemba 13, mwaka huu.
Kwa ujumla,Ronaldo anafikisha mabao 948 katika Maisha yake ya soka, pia 143 akiwa na jezi za timu ya taifa.
Katika miaka yake 22 akiwa na Ureno, ameiwezesha kutwaa taji la Mataifa ya Ulaya (Euro) mwaka 2016 na Ligi ya Mataifa ya Ulaya (Uefa Nations League) mara mbili.
Je, ataiongoza Ureno kukata tiketi ya kushiriki fainali zijazo za Kombe la Dunia za mwakani? Majibu ni Novemba 13.

Related articles

Recent articles