24.8 C
New York

Qatar yaandika historia Kombe la Dunia

Published:

DOHA, Qatar
HII inakuwa mara ya pili kwa Qatar kushiriki Kombe la Dunia lakini ni mara ya kwanza kukata tiketi kupitia mechi za kufuzu.
Ikumbukwe, Qatar ilikuwa mwenyeji a Kombe la Dunia mwaka 2022, hivyo ilipata mteremko wa kutokucheza mechi za kuwania tiketi.
Safari hii, Taifa hilo la Kiarabu limekata tiketi kwa kuvuja jasho baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), wafungaji wake wakiwa ni Boualem Khoukhi na Pedro Miguel.
Ikumbukwe, Qatar ikiwa nyumbani ilimaliza mchezo huo ikiwa na wachezaji 10 uwanjanui baada ya Tarek Salman kulimwa kadi nyekundu katika dakika ya 87.
Ushindi huo umeifanya Qatar kufuzu ikiwa kileleni mwa msimamo wa Kundi A, huku UAE iliyoshika nafasi ya pili ikiangukia ‘playoffs’, wakati huo Oman iliyopo nafasi ya tatu ikiondoshwa kabisa.
Ikiwa mwenyeji wakati ule wa fainali za mwaka 2022, Qatar iliishia makundi ikiwa imepoteza mechi zote tatu za hatua hiyo.

Related articles

Recent articles