24.8 C
New York

Wilshere kupewa kazi Daraja la Pili England

Published:

LONDON, Uingereza
KIUNGO wa zamani wa Arsenal, Jack Wilshere, huenda akatangazwa kuwa kocha mkuu wa Luton Town ya Ligi Daraja la Pili ya England.
Luton wameuanza vibaya msimu huu wa 2025-26 kwani wameshafungwa mechi tano kati ya 11 na wanashika nafasi ya 11 katika msimamo wa Ligi.
Bodi ya klabu hiyo imeripotiwa kuanza mazungumzo na Wilshere mwenye umri wa miaka 33 baada ya kumfuta kazi Matt Bloomfield mapema wiki hii.
Mara ya mwisho kwa Wilshere kuwa kazini katika majukumu ya ukocha ni msimu uliopita, ambapo aliiongoza Norwich City katika mechi mbili za mwisho baada ya Johannes Hoff kutimuliwa.
Kabla ya kwenda kuwa msaidizi katika klabu ya Norwich, Wilshere alikuwa kocha wa timu ya vijana wa U-18 ya Arsenal.
Itakumbukwa, alicheza mechi 34 akiwa na timu ya taifa ya England, pia akiitumikia Arsenal mara 197, kabla ya kutimkia West Ham na Bournemouth.

Related articles

Recent articles