24.8 C
New York

Haaland afikisha ‘hat trick’ sita, mabao 51 Norway

Published:

LONDON, Uingereza
KATIKA mechi saba pekee za mwanzoni mwa msimu huu wa Ligi Kuu ya England (EPL), Erling Haaland ameshaifungia Manchester City jumla ya mabao tisa.
Wakati wengi wakimuona ni wa moto, takwimu zinaonesha kuwa bado hapo Haaland hajawa kwenye kiwango chake bora.
Ni kawaida yake. Msimu uliopita, baada ya mechi saba za mwanzo, alishafunga mabao 10.
Kwa sasa, si tu anaongoza mbio za ufungaji bora kwa tofauti ya mabao matatu, pia hakuna alilofunga kwa mkwaju wa penalti.
Wakati huo huo, Haaland ndiye kinara wa mashuti msimu huu wa Ligi Kuu ya England (EPL). Ameshapiga mashuti 29, huku asilimia 27 yakisabanisha mabao aliyofunga.
Kwa ujumla, Haaland amezipasia nyavu katika mechi zote 10 alizocheza hivi karibuni akiwa na Man City na timu ya taifa ya Norway.
Baada ya ‘hat-trick’ yake katika ushindi wa 5-0 dhidi ya Israel jana, amefikisha mabao 51 katika mechi 46 alizoitumikia timu yake hiyo ya taifa.
Pia, ukiacha Cristiano Ronaldo na Lionel Messi, Haaland ndiye mchezaji pekee mwenye ‘hat-trick’ nyingi (6) akiwa na timu ya taifa.

Related articles

Recent articles