SHANGHAI, China
MASTAA wawili wa mchezo wa tenesi, Novak Djokovic na Daniil Medvedev, wameshindwa kutinga fainali ya michuano ya Shanghai Masters.
Katika mchezo wa nusu fainali wa jana, Djokovic raia wa Serbia alifungasha virago baada ya kufungwa na Valentin Vacherot.
Vacherot raia wa Ufaransa, ambaye anashika nafasi ya 204 katika viwango vya ubora duniani, alimchapa Djokovic kwa seti 6-3 6-4.
Djokovic mwenye umri wa miaka 38, alilazimika kufanyiwa matibabu mara kadhaa wakati mchezo huo ukiendelea, ikikumbukwa pia alitapika katika mechi iliyopita.
Kwa upande wa Medvedev, ambaye ni bingwa wa michuano hiyo mwaka 2019, jana alipoteza nusu fainali yake mbele ya Arthur Rinderknech.
Rinderknech mwenye umri wa miaka 30, hakupewa nafasi kubwa ya kushinda mchezo huo lakini haikumzuia kumtandika staa huyo kwa seti 6-4, 6-2 6-4.
Published:


